Jumamosi 18 Julai 2026 - 13:55
Baadhi wanapaswa kujinasua kutoka katika dhana potofu ya kushikamana na mazungumzo yasiyo na manufaa na yenye madhara

Hawza/ Imamu wa Swala ya Ijumaa wa mji wa Qum amesema: Baadhi wanapaswa kujinasua kutoka katika dhana potofu ya kushikamana na mazungumzo yasiyo na manufaa na yenye madhara, kwa kuwa kufanya mazungumzo na adui ambaye lengo lake ni kuuangusha Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu hakuna faida yoyote, na amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kusimama katika nafasi ya udhaifu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saiidi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qum, katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 26 Tir (July 17 2026), zilizofanyika katika Muswalla Quds, alisema: Mazishi ya kihistoria, ya ustaarabu na yasiyo na mfano ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi yalikuwa hatua muhimu katika historia. Ushiriki wa takribani watu milioni 43 katika siku zenye joto kali zaidi la mwaka, kwa muda wa mchana na usiku kadhaa nchini Iran na Iraq, unaonesha namna Imam Shahidi alivyoitawala mioyo na nafsi za mamilioni ya watu katika karne mbalimbali.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qum aliongeza: Mazishi hayo makubwa yalidhihirisha kuibuka kwa dola kuu ya kiroho, ya kiimani na ya wananchi, na yakawa hatua muhimu katika harakati za ustaarabu za taifa la Iran na Mhimili wa Muqawama. Vipengele vyake vya kisiasa, kijamii, kiusalama, kitamaduni na kiutawala ni miongoni mwa sifa za utawala unaozingatia Wilayah, ambao haujawahi kuwa na mfano katika historia ya dunia.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, huku akivishukuru vikosi vya ulinzi, alionya: Jibu kali la wapiganaji wetu dhidi ya adui asiye na dhamiri, asiye na akili na mwenye tabia ya kucheza kamari lilikuwa na ujumbe ulio wazi.

Ayatullah Saiidi alisisitiza: Tunazikumbusha nchi za Kiislamu za eneo hili kwamba zisipelekee heshima ya ardhi za Kiislamu kuchafuliwa kwa uwepo wa makafiri wahalifu wa Marekani na Kizayuni, wala zisiruhusu ardhi zao zitumike kutekeleza uhalifu dhidi ya wananchi wa Palestina, Lebanon, Iran na Yemen.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qum akizungumzia mazungumzo na adui alisema: Baadhi wanapaswa kujinasua kutoka katika dhana potofu ya kushikamana na mazungumzo yasiyo na manufaa na yenye madhara, kwa kuwa kufanya mazungumzo na adui ambaye anafikiria kuuangusha Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu hakuna faida yoyote, na amani ya kweli haiwezi kupatikana kwa kusimama katika nafasi ya udhaifu.

Msimamizi wa Haram ya Bibi Masumah (as) alisema: Popote tuliporudi nyuma, adui alizidi kuwa jeuri; na kila tuliposimama imara, alilazimika kurudi nyuma. Hivyo, taifa letu halitarudi nyuma kamwe kutoka katika Muqawama, na leo sauti yoyote itakayojaribu kuhalalisha kurudi nyuma kwa jina la busara inapaswa kulaaniwa.

Akirejelea utayari wa kijeshi, alisisitiza: Vikosi vya ulinzi vinapaswa kuongeza kasi ya maandalizi ya vita na kupanua benki yao ya malengo, kwa namna ambayo pigo litakalompata adui lisiloweza kufidiwa. Orodha kuu ya malengo hayo inajumuisha visima vya mafuta na miundombinu ya nishati katika eneo hili inayohusiana na utawala wa Kizayuni na Marekani.

Ayatullah Saiidi alionya kuhusu vitisho vya Trump na kusema: Endapo jeshi la kigaidi la Marekani litafanya kosa la kimkakati, basi kila mtu ajue kwamba katika hali hiyo hakuna yeyote atakayekuwa na haki ya kutumia nishati ya eneo hili. Sera thabiti ya Iran ni hii: ima nishati kwa wote, au isiwe kwa yeyote.

Muqawama ndiyo njia pekee ya kuyakomboa mataifa ya eneo hili

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qum akizungumzia Muqawama wa Lebanon alisema: Kinachoendelea nchini Lebanon ni vita kati ya nguvu ya kiburi na irada ya waumini. Adui anataka kuwatia hofu wananchi, lakini Muqawama unazidi kuimarika kwa kila pigo linaloupata, njia pekee ya wokovu ni kushikamana na Tawhidi na Muqawama, kisha akasoma kauli ya Mwenyezi Mungu:

«إِنَّ الَّذِینَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَیْهِمُ الْمَلَائِکَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا»

Alisisitiza: Kinachoendelea leo nchini Lebanon si mapambano ya kijeshi pekee, bali ni vita kati ya irada ya waumini na kambi ya ubeberu.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qum aliongeza: Adui, kwa kutumia mbinu kama mauaji ya kigaidi, uharibifu na vitisho, anataka kuivunja irada ya wananchi wa Lebanon na Muqawama wa Kiislamu, hata hivyo, uzoefu umeonesha kuwa Muqawama huzidi kuota mizizi na kuwa imara zaidi kwa kila shinikizo linaloukumba.

Aliendelea kusema: Lebanon leo inayafundisha mataifa ya eneo hili kwamba njia pekee ya kukabiliana na wavamizi na wavunjaji wa ahadi ni kushikamana na imani, Muqawama na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Kiongozi Shahidi alikuwa ni neema ambayo ukubwa wake ulidhihirika zaidi baada ya kufariki kwake

Aidha, alitoa mkono wa pole kwa maadhimisho ya kumbukumbu ya shahada ya Bibi Ruqayyah (as), na kuheshimu kumbukumbu ya mashahidi wa hivi karibuni, mashahidi wa Shule ya Mina na mjukuu wa Imam wa Umma.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qum pia, akirejelea kumbukumbu ya shahada ya Imam Hasan Mujtaba (as), alinukuu riwaya kutoka kwake kuhusu namna neema zinavyobaki kutojulikana hadi pale zinapopotea. Alisema: Uwepo wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa watu wengi kabla ya shahada yake haukutambulika ipasavyo kama ulivyostahili, lakini baada ya shahada yake, athari na baraka za uwepo wake zilidhihirika zaidi kuliko hapo awali, na watu wakatambua ni johari yenye thamani kubwa kiasi gani waliyoipoteza.

Aidha, aliwataka wananchi wamfuate Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusisitiza umuhimu wa kusikiliza na kufuata maelekezo yake.

Kukabiliana na vita laini kunahitaji kuimarisha imani na kuchukua hatua madhubuti

Ayatullah Saiidi, katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alisema kuwa; kuenezwa kwa maadili yaliyopotoka, kutoheshimu hijabu, matumizi ya dawa za kulevya na vileo ni sehemu ya vita laini vya adui vinavyolenga kudhoofisha misingi ya dini na familia.

Alisema: Lengo la adui kupitia hatua hizi ni kufifisha utambulisho wa kidini na wa kitaifa wa jamii na kuandaa mazingira ya kupenya kiutamaduni na kisiasa.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Qum alisisitiza: Kukabiliana na njama hii kunahitaji kuimarisha imani, kuongeza uelewa wa umma na hatua madhubuti za viongozi dhidi ya maovu, kutoheshimu hijabu na uenezaji wa dawa za kulevya.

Mwishoni mwa hotuba yake, Ayatullah Saiidi alirejea tena mazishi makubwa ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuelezea kuwa ushiriki huo wa kipekee wa wananchi ulikuwa hatua muhimu katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu na ishara ya nguvu ya kiroho, ya wananchi na ya ustaarabu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Alisema: Kuagwa huku kwa kihistoria ilikuwa ni taswira ya uhusiano wa kina kati ya taifa na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na Mhimili wa Muqawama.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha